About Me

YERICKO NYERERE AKAMATWA AKIWA NYUMBANI KWAKE. WACHUKUA SIMU NA LAPTOP

Watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi kitengo cha cyber crime! Wamefika mda huu majira ya saa 7:04 usiku, Kwa Yericko Nyerere wakiambatana na mwenyekiti Wa mtaa (Mbutu), walipofika wamemchukua yeye pamoja na vifaa vyake ikiwemo simu na laptop yake na kuondoka naye kuelekea kituo cha police kigamboni wakimtuhumu kuhusika na kosa la kimtandao.(ingawa hawakueleza kosa halisi kafanya lini na wapi).

Taarifa zaidi mtaendelea kuzipata baadae.
Ikumbukwe hii ni Mara ya pili kukamatwa kwake, baada ya kesi yake iliyodumu Kwa miaka miwili tangu kipindi cha uchaguzi ambapo alishinda na kuachiwa huru mapema April 2017.

No comments:

Powered by Blogger.